Aliyekuwa mgombea mwenza wa Azimio Martha Karua amezindua chama kipya cha People's Liberation Party (PLP) katika makao makuu jijini Nairobi.
Chama hicho kilizinduliwa kuchukua nafasi ya chama cha awali cha Narc Kenya chama ambacho kilikuwepo kwa miongo zaidi ya miwili.
PLP ni chama ambacho kilizinduliwa kwa misingi ya Demokrasia,uwajibikaji
na Usawa maelezo ya dibaji ya chama hicho yalieleza. Vilevile chama hicho kilizinduliwa na kauanzisha uongozi wa
mihula kwa kiongozi wa chama.
Chama hicho kiliasisiwa kwa vigezo maalum vya kuendeleza
uongozi ambao unaajibikia matakwa ya wananchi na kuipa kipaumbele kauli ya chama ambayo ni Kuungana na kukomboana.
Baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa
chama hicho ni Kinara wa Wiper Daktari Stephine Musyoka,Eugine Wamalwa,Rigathi
Gachagua,Morara Kebaso,Jimmy Wanjigi,Mukhisa Kituyi na Kivutha Kibwana.
Katika usemi wake Eugine Wamalwa aliwarai vijana wa kisasa
wa Gen Z kuwaunga mkono ili wakomboe nchi kutoka kwa utawala mbaya wa rais William Ruto
akisema kuwa ukombozi huo utajumuisha vijana,kanisa na viongozi wote.
Kwa upande wake kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alitoa
pendekezo la kuirasimisha tarehe 25 Juni
kila mwaka kuwa kama siku ya Kitaifa kwa kumbukumbu za kuwakumbuka na kukumbuka
kazi waliotekeleza vijana wa Gen Z kwa kuandamana na kupinga uongozi mbaya tena wa
kidekteta.
Alimpongeza sana kinara wa PLP Martha Karua kwa kuzindua
chama na kuanzisha nuru na mwanga katika ukombozi wa taifa.
Aliyekuwa Naibu wa rais Rigathi Gachagua alisema kuwa
kutokana na wingi wa watu waliwarai wamtume nyumbani mara moja Rais Ruto Pamoja na utawala wake wa
kiimla.
Rigathi Gachagua alisema chini ya muda wa miaka miwili serikali ya Kenya Kwanza ilisambaratisha Hospitali,elimu na Uchumi.
Katika usemi wa Rigathi Gachagua alisema kuwa kule Kareni kwa
Naibu wa Rais Kithure Kindiki kulikuwa na bomba la kuhifadhi pesa ambalo lilikuwa limewekwa pale kwa minajili
ya kuhonga watu ambao wanahudhuria mikutano.
Vilevile Gachagua alisema kuwa kule Ikulu kulikuwa na bomba
la kuhifadhia pesa aina ya dola kwa
kuwalipa na kuwahonga viongozi mbalimbali,vilevile alisema kuwa kuna Memo au
arifa ambayo ilioandikwa itakayopelekwa
katika baraza la Magavana ili mashamba ya majela yauziwe wawekezaji.
Kwa upande wake Martha Karua alisema kuwa serikali ilikuwa
ikibomoa nyumba za walalahoi na kuwapa wandani wake,alimkanya kiongozi wa taifa kuwacha kuwateka nyara
wageni wa nchi za kigeni kwa kuungana na kuwateka nyara wananchi kutoka mataifa
ya jumuiya ya Afrika Mashariki .
Aliwakumbusha kuwa mamlaka ya viongozi wa serikali yote upo kwa
mwananchi mpiga kura wala si kwa nguvu
zao kama viongozi.